Tarehe 26 Februari 2024, Mhe. Maj. Gen. Paul Kisesa, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Uganda alifanya Ziara ya kutembelea Kiwanda cha Bakhresa Grain Milling (Uganda) Limited (BGM Uganda) kinachozalisha unga wa ngano wenye chapa ya Azam. Kiwanda hicho kinamilikiwa na Mtanzania, Bw. Salim Bakhresa. Ziara hiyo ilifanyika ikiwa ni sehemu ya mpango wa Ubalozi wa kutembelea biashara, makampuni na wawekezaji wa Kitanzania waliopo nchini Uganda.