Mhe. Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Uganda alifanya Ziara ya kutembelea Kiwanda cha CIPLO kilichopo Kampala iliyofanyika tarehe 3 Mei 2024.  Kiwanda cha CIPLO ni kiwanda kinachozalisha dawa za binadamu kama vile za kutibu malaria, VVU na figo. Ziara hiyo ilifanyika kufuatia mwaliko kutoka kwa Mheshimiwa Kanali Mstaafu Fred Mwesigye, Balozi wa Jamhuri ya Uganda katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kuona shughuli mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo na kutoa mwaliko rasmi wa kushiriki katika Kongamano la Biashara kati ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania na Jamhuri ya Uganda linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam, tarehe 23 na 24 Mei 2024. 
Ujumbe uliofika katika ziara hiyo uliweza kutembelea eneo lote la kiwanda na kuona shughuli mbalimbali zinazoendelea katika eneo hilo.