Mhe. Maj. Gen. Paul Kisesa Simuli, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda alifanya ziara ya kikazi Hoima, Uganda tarehe 15 na 16 Mei, 2024. Ziara ililenga kutembelea miradi ya uchimbaji wa mafuta ya kingfisher; Tilenga; na Eneo la Viwanda la Kabalenga/Kabaale katika Wilaya ya Hoima na Buliisa. Miradi hii ni muhimu kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda kwa kuwa bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) litasafirisha mafuta yatakayochimbwa katika eneo hilo mpaka Chongoleani, Tanga.



