Mhe. Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Uganda alifanya Ziara ya kutembelea Kiwanda cha Kiira Motors Corporation kilichopo Jinja tarehe 2 Mei 2024.
Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kuona shughuli mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo na kutoa mwaliko rasmi wa kushiriki katika Kongamano la Biashara kati ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania na Jamhuri ya Uganda linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam, tarehe 23 na 24 Mei 2024.



