Tarehe12 Mei 2024, Ubalozi ulishiriki katika kikao cha Diaspora wa Tanzania waishio Jinja. Pamoja na masuala mengine, Mhe. Maj. Gen. Paul Kisesa Simuli, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Uganda alitumia nafasi hiyo kujitambulisha; kuongea nao masuala mbalimbali yanayohusu diaspora; kusikiliza na kujibu changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Diaspora walimshukuru Mhe. Balozi kwa kuweza kukutana nao; aidha, walitoa historia fupi ya Umoja wao ulioundwa 2019. Walieleza faida mbalimbali wanazozipata kutokana na umoja huo ikiwemo kusaidiana wenyewe kwa wenyewe katika shida na raha.



