Sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa Bomba Ghafi la Mafuta la Afrika Mashariki (EACOP) zilifanyika tarehe 09 Novemba, 2017 ambapo Watanzania (Diaspora) wanaoishi Uganda walishiriki katika sherehe hizo. Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mheshimiwa Rais Yoweri Museveni waliwasalimia Watanzania hao waliposhiriki kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Wilaya ya Kyotera, Uganda.
