Tarehe 23 Septemba 2022, Mheshimiwa Dkt. Aziz Ponary Mlima, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Uganda alizindua Klabu ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbarara (MUST), Uganda. Sherehe hizo zilifanyika sambamba na Sherehe za kuwakaribisha wanafunzi kutoka nje ya Uganda ambao wamejiunga na Chuo hicho.
Klabu hiyo itatoa fursa kwa wanafunzi wanaosoma Chuoni hapo kujifunza lugha ya Kiswahili.
Ni vyema ikafahamika kwamba ufunguzi wa vilabu vya Kiswahili katika Vyuo Vikuu vya nchini Uganda ni miongoni mwa mikakati ya Ubalozi katika kukuza matumizi ya Lugha ya Kiswahili nchini Uganda.

