Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi leo Jumapili, tarehe 9 Oktoba 2022, amemuwakilisha Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Jamhuri ya Uganda zilizofanyika katika uwanja wa Kololo, Jijini Kampala.
Pamoja na viongozi wengine, Mheshimiwa Rais Mwinyi aliambatana na mke wake, Mama Mariam Mwinyi; na Mheshimiwa Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.