Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 21 February, 2018 amewasili nchini Uganda ambapo atahudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaofanyika Ijumaa tarehe 23 February, 2018 Mjini Kampala.
Katika uwanja wa ndege wa kimataifa Mhe. Rais Magufuli amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa UgandaMhe. Sam Kutesa na kisha kuelekea Ikulu ya Entebbe ambako amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.
Kesho tarehe 22 February, 2018 Mhe. Rais Magufuli atahudhuria mkutano maalum katika ngazi ya wakuu wa nchi unaohusu masuala ya miundo mbinu na afya na keshokutwa trarehe 23 February, 2018 na atahudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na ujumbe wake katika Mazungumzo na Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitaabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitaabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya mazungumzo yao katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebe nchini Uganda ambapo pamoja na mambo mengine atahudhuria vikao vya Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki vitakavyoanza kesho jijini Kampala nchini Uganda.
Kikundi cha ngoma za Asili cha Masters of ground kutoka Wilaya cha Kyotera, Masaka nchini Uganda wakitumbuiza mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebe nchini Uganda. PICHA NA IKULU
