Tarehe 22 Agosti, 2018 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi akisoma hotuba ya ufunguzi ya Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Uganda kwa ngazi ya Makatibu Wakuu alieleza kuwa tokea JPC kati ya Tanzania na Uganda ilipoanzishwa mafanikio makubwa yamepatikana. Mafanikio hayo ni pamoja na kusainiwa kwa mikataba ya makubaliano mbalimbali ikiwemo mkataba wa kushirikiana katika ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Kikagati/Murongo na makataba wa kushirikiana katika usafiri wa anga ambapo Tanzania inakusudia kuanza safari za moja kwa moja kutoka Dar Es Salaam kwenda Kampala hivi karibuni. 

  • Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia kwa makini hotuba ya Balozi Mwinyi
  • Ujumbe wa Uganda ukifuatilia hotuba za ufunguzi zilizokuwa zinasomwa na Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje za Tanzania na Uganda