Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Uganda uliandaa sherehe za Siku ya Kiswahili duniani zilizofanyika tarehe 7 Julai, 2022 katika viwanja vya Ubalozi. 

 

Wadau mbalimbali wa Kiswahili nchini Uganda walipata fursa ya kushiriki katika sherehe hizo wakiwemo wadau kutoka Serikali ya Uganda, Mabalozi na Wakuu wa Jumuiya za Kimataifa nchini Uganda, wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali ambao wanasoma katika shule na Vyuo Vikuu vya Uganda.

 

Mgeni rasmi katika sherehe hizo alikua Mhe. Peace R. Mutuuzo, Waziri wa Nchi, Jinsia na Utamaduni wa Jamhuri ya Uganda. Wakati akitoa hotuba yake Mhe. Waziri Mutuuzo aliwahakikishia washiriki kwamba Serikali ya Uganda itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha lugha ya Kiswahili inaendelea kukua nchini Uganda.

 

Kwa upande wake, Mhe. Dkt. Aziz P. Mlima, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Uganda alisisitiza kwamba lugha ya Kiswahili haina mwenyewe na hiyo ni moja ya lugha za Kiafrika ambayo ni lugha unganishi. Kwa msingi huo, mtu yeyote anaweza kujifunza na kutumia kwenye shughuli mbalimbali kama vile za kijamii, kisiasa na kiuchumi. Aidha, aliwaomba washiriki kushirikiana kwa pamoja ili kuikuza lugha ya Kiswahili ambayo inaendelea kuliunganisha bara la Afrika na dunia kwa ujumla. 

 

Sherehe hizo zilipambwa na matukio mbalimbali yenye maudhui ya lugha ya Kiswahili kama vile ngonjera, maigizo, mashairi, na mdahalo.

  • Pichani ni  baadhi ya washiriki wakifuatilia matukio mbalimbali katika siku ya Kiswahili duniani katika viwanja vya Ubalozi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda.Pichani ni baadhi ya washiriki wakifuatilia matukio mbalimbali katika siku ya Kiswahili duniani katika viwanja vya Ubalozi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda.
  • Wanafunzi kutoka Chuo kikuu cha Makerere wakiimba shairi katika siku ya kiswahili Duniani.Wanafunzi kutoka Chuo kikuu cha Makerere wakiimba shairi katika siku ya kiswahili Duniani.
  • Baadhi ya washiriki wa mdahalo  uliofanyika katika  siku ya Kiswahili Duniani.Baadhi ya washiriki wa mdahalo uliofanyika katika siku ya Kiswahili Duniani.
  • Pichani ni  baadhi ya washiriki wakifuatilia matukio mbalimbali katika siku ya Kiswahili duniani katika viwanja vya Ubalozi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda.Pichani ni baadhi ya washiriki wakifuatilia matukio mbalimbali katika siku ya Kiswahili duniani katika viwanja vya Ubalozi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda.