Baadhi ya mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali akiwemo Mhe. Dkt. Aziz Ponary Mlima, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda, wameshiriki zoezi la kupanda Mlima wa Kilimanjaro (Kill Climb 2022) ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono Juhudi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kukuza Utalii wa ndani na nje ya nchi. Zoezi hilo limeandaliwa na kuratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), TANAPA ,KINAPA, Zara adventures na Mabalozi wa Tanzania.